Wakili George Kithi atwaa Uenyekiti wa Hazina na SASDF

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakili George Kithi amekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa hazina ya maendeleo ya michezo na Sanaa (SASDF) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kithi amerithi wadhfa huo kutoka kwa Rais wa chama cha Riadha Kenya, Jackson Tuwei, ambaye amekuwa mwenyekiti tangu mwaka 2019.

Hafla ya kukabidhiwa mamlaka imeandaliwa Jumatano kwenye makao makuu ya Wizara ya Michezo na kushuhudiwa na Waziri Salim Mvurya.

Kithi aliteuliwa mwenyekiti wa hazina ya SASDF tarehe 6 mwezi jana na Rais William Ruto.

Hazina hiyo hujukumika  na ugavi wa pea kwa mashirikisho ya michezo, shughuli za ukuzaji talanta na hafla za kitaifa za kitamaduni.

Share This Article