Wakfu wa Eliud Owalo watoa msaada kwa timu ya vijana ya Muhoroni

Marion Bosire
1 Min Read

Asubuhi ya leo, waziri wa mawasiliano na uchumi dijitali Eliud Owalo leo aliandaa mashauriano na usimamizi wa timu ya soka ya Muhoroni Youth na hata wachezaji wa timu hiyo katika uwanja wa Muhoroni katika kaunti ya Kisumu.

Baada ya mashauriano hayo waziri Owalo kupitia kwa wakfu wake alitoa msaada wa sare za mazoezi 40 na pesa taslimu laki 5 kwa timu hiyo.

Courtesy of the Eliud Owalo Foundation, we have donated 40 Tracksuits plus a Cash donation of Ksh. 500,000 to the team.

Waziri huyo alisema kwamba kutambua na kukuza talanta za vijana kupitia michezo kwa ajili ya kuwapa uwezo kiuchumi ni mojawapo ya malengo makuu ya serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na Rais William Ruto chini ya mpango wa Bottom Up Economic Transformation Agenda(BETA).

Owalo alikuwa ameandamana na seneta wa kaunti ya Kisumu Profesa Tom Ojienda, mwenyekiti wa mamlaka ya kudhibiti vyama vya akiba na mikopo SASRA Jack Ranguma, Mkurugenzi wa mamlaka ya kilimo na chakula nchini AFFA Samwel Ongow, aliyekuwa waziri msaidizi Profesa Ayiecho Olweny na aliyekuwa Meya wa jiji la Kisumu Sam Okello kati ya wengine wengi.

Share This Article