Wakenya wanaoishi ng’ambo watuma nchini shilingi bilioni 48.8

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakenya wanaoishi ughaibuni walituma nchini shilingi bilioni 48.8 mwezi Juni mwaka huu.

Hii ni kulinganisha na shilingi bilioni 49.6 walizotuma mwezi Mei.

Hatua hiyo inamaanisha kiwango cha fedha zilizotumwa nchini mwezi Juni kilipungua kwa asilimia 1.6 ikilinganishwa na mwezi jana.

Licha ya kupungua kwa kiwango hicho mwezi hadi mwezi, data za hivi karibu kutoka kwa Benku Kuu Nchini, CBK zinaashiria kuwa mtiririko wa fedha zilizotumwa uliongezeka kwa asilimia 6.1 mwezi Juni mwaka huu ikilinganishwa na mwezi sawia mwaka jana wakati ambapo raia wanaoishi ng’ambo walituma nchini juma ya shilingi bilioni 46.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *