Wakenya wanaoishi Lebanon watakiwa kujisajili haraka ili kuhamishwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali imewataka Wakenya wanaoishi nchini Lebanon kujisajili haraka ili kuwezesha kuhamishwa kwao kutoka nchini humo. 

Wanaotaka kujisajili wanaweza kufanya hivyo kupitia linki ifuatayo: https://tinyurl.com/2m9nw4ww au kupiga simu kupitia nambari +96590906719/ +96171175006/ +254114757002 kwa ajili ya kuhamishwa kutoka nchini humo.

“Tunatoa wito kwa wale wanaoweza kuhamia maeneo salama ndani ya Lebanon na wale wanaoweza kuondoka nchini humo kufanya hivyo,” imesema Wizara ya Mambo ya Nje katika taairifa.

Taarifa hiyo inafuatia mzozo unaozidi kuongezeka Mashariki ya Kati hususan kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hezbollah.

Marekani, Uingereza na Ufaransa ni miongoni mwa nchi ambazo pia zimewataka raia wake kuondoka nchini Lebanon huku kukiwa na wasiwasi ya kuongezeka kwa mzozo Mashariki ya Kati.

Ripoti zinaashiria kuwa Iran na Hezbollah zinapanga kuishambulia Israel katika hatua ambayo huenda ikaongeza mzozo Mashariki ya Kati.

 

Share This Article