Wakenya walimiminika katika maeneo mbalimbali kote nchini kuukaribisha mwaka mpya 2025.
Wapo waliokuwa kwenye kesha kuhudhuria ibada katika makanisa mbalimbali,tamasha za muziki nao wengine walifurika barabarani kwa vifijo,shangwe na nderemo kwa kumaliza mwaka 2024 salama na kuvuka mwaka mya wa 2025.
Katika mitaa mbalimbali ya kifahari baruti zilisheni angani kwa kutoa rangi tofauti .
Mwaka mpya wengi walijawa na matumaini ya kuwa mwaka bora kuliko mwaka jana.
Rais William Ruto aliwaongoza Wakenya kwa hotuba ya mwaka mpya kutoka ikulu ndogo ya Kisii.
Eneo la Kiritimati lilikuwa la kwanza kuvuka mwaka mpya ikifuatwa na New Zealanda na Japan mtawalia.