Wakenya wanaoishi ughaibuni walituma nyumbani shilingi bilioni 54 nukta 6 mwezi Julai mwaka huu ikiwa ongezeko la asilimia 18 nukta 4, kutoka kwa bilioni 46 nukta 1 zilizotumwa Julai mwaka 2021.
kulingana na wataalamu wa maswala ya kifedha kiwango hicho kiliongezeka kutokana na kudorora kwa shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Marekani.
Pia kiwango cha pesa zilitumwa na Wakenya kutoka ughaibuni hadi nyumbani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kiliongezeka kwa asilimia 2 kutoka bilioni 576 hadi bilioni 588 nukta 4 .