Serikali imejitolea kuwatafutia vijana nafasi za ajira, asema Dkt. Mutua

Tom Mathinji
2 Min Read
Waziri wa leba na ulinzi wa jamii, Dkt. Alfred Mutua.

Waziri wa leba na ulinzi wa jamii Dkt. Alfred Mutua, amsema serikali inatia bidii katika kuwatafutia ajira hapa nchini na katika ngazi za kimataifa.

Waziri huyo alidokeza kuwa, serikali ya Rais William Ruto hadi kufikia sasa imetafuta maelfu ya nafasi za ajira katika masoko ya kimataifa, licha ya kwamba vijana wengi wanakosa fursa hizo kutokana na changamoto za kifedha.

“Ili kushughulikia changamoto hii, hazina ya vijana imebuni aina ya mkopo ya hadi shilingi 300,000 kwa vijana ambao wamepata ajira katika Muungano wa Milki za Kiarabu na mataifa mengine lakini hawana fedha za kugharamia visa, nauli na mahitaji mengine,” alisema Dkt. Mutua.

Kulingana na Mutua, hatua hiyo itapunguza pengo la kifedha na kuhakikisha hakuna kijana atakosa fursa za ajira kutokana na ukosefu wa fedha.

Aidha alitoa wito kwa kampuni zinazowaajiri vijana kufanya kazi ughaibuni, kutekeleza shughuli hiyo kwa maadili ya hali juu.

“Ikiwa kampuni itamsajili anayetafuta ajira na kazi hiyo isipatikane, basi ni bora kwa kampuni hiyo kumrejeshea fedha zake aliyekuwa akitafuta ajita hiyo.

Aliyasema hayo alipoongoza sherehe za maonyesho ya kutangaza nafasi za ajira katika kaunti ya Garissa.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Gavana wa Garissa Nathif Jama, wawakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO), maafisa wa serikali, wadau kutoka sekta ya kibinafsi na washirika wengine muhimu wanaounga mkono utafutaji nafasi za ajira na uimarishaji uchumi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article