Wakenya sasa kuutazama mwili wa ‘Baba’ uwanjani Kasarani

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya sasa watautazama mwili wa marehemu Raila Odinga leo Alhamisi katika majengo uwanja wa michezo wa Kasarani.

Hii ni baada ya mipango ya awali ya kuutaza mwili huo katika majengo ya bunge kubadilishwa.

Hatua hiyo ilitokana na idadi kubwa ya Wakenya waliojitokeza kuupokea mwili wa Raila katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.

Idadi hiyo ikifanya iwe vigumu kufuata ratiba ya awali kiasi kwamba hata mwili haukupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee.

Awali, Wakenya walipangiwa kuutazama mwili wa Raila katika majengo ya bunge.

Mazishi ya kitaifa yatakayoongozwa na serikali yataandaliwa kuanzia saa mbili asubuhi kesho Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Baadaye, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake mtaani Karen kwa mkesha kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Bondo siku ya Jumamosi utakapolazwa nyumbani kwake kwa mkesha kabla ya kumpuzishwa siku ya Jumapili.

Serikali ilitangaza maombolezi ya kitaifa ya siku saba kuanzia Alhamisi huku bendera ya kitaifa ikipeperushwa nusu mlingoti katika balozi za Kenya na afisi zote za umma kote nchini.

Website |  + posts
Share This Article