Wakenya nchini Lebanon wahimizwa kujisajili ili wahamishwe

Tom Mathinji
1 Min Read
Shambulizi la Israel nchini Lebabon

Serikali imetoa wito kwa raia wa Kenya walioko nchini Lebanon kujisajili ili wahamishwe, huku Israel ikiendelea kushambulia taifa hilo.

Hadi kufikia sasa Umoja wa Mataifa umesema takriban watu Milioni moja wameachwa bila makazi kutokana na vita hivyo.

Taarifa kutoka idara ya maswala ya ughaibuni, ilisema siku ya mwisho kwa Wakenya hao kujisajili ni Oktobta 12, 2024.

“Ili kuhakikisha usalama na shughuli ya kuwahamisha raia wetu kwa wakati, tunawahimiza wakenya wote walio nchini Lebanon kujisajili mara moja. Ni wakenya tu waliojisajili ndio watahamishwa,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa Oktoba 1,2024.

Aidha kulingana na taarifa hiyo, serikali tayari imehamisha makundi mawili ya raia wa Kenya kutoka Lebanon, ikisema itaendelea na juhudi za kuwaokoa hadi Wakenya wote watakapookolewa.

Hata hivyo, idara hiyo ilisikitika kuwa idadi kubwa ya wakenya bado hawajajisajili kuhamishwa, licha ya kuhimizwa kufanya hivyo mara kadhaa.

Wale wanaotaka kuhamishwa wanapaswa kujisajili kupitia https://www.diaspora.go.ke/lebanon.html, au idara ya mawasiliano na ushirikishi kupitia  +96590906719,

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article