Wizara ya Afya imetangaza kuwa jumla ya Wakenya 12,704,548 wamehamia kwa Bimpa mpya ya Afya ya Jamii, ya SHIF chini ya Mamlaka ya Afya nchini, SHA kufikia Jumapili.
Katibu katika Wizara hiyo Harry Kimtai ametangaza hayo Jumapili ikiwa siku ya sita tangu kuzinduliwa kwa mpango wa usajili wa kitaifa.
Wafanyakazi 10,904 pia wamepewa mafunzo katika mchakato huo wa kuhamisha na kuwasajili Wakenya katika bima hiyo mpya.
Kulingana na Katibu Kimtai, waliojisali kwa bima mpya watapokea matibabu katika hospitali na zahanati za Level 2, Level 3 na 4 pamoja na hospitali za umma za Level 2 hadi Level 6.
Jumla ya vituo vya afya 1,442 vya kidini vimejiandikisha na SHA.