Wakenya hawatahitaji VISA tena kusafiri kuingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya serikali ya DR Congo kuondoa sharti ya viza kwa raia wa Kenya.
Haya yanajiri wiki moja pekee baada ya Kenya kuondoa masharti ya viza kwa raia wa Congo wanaozuru Kenya, kama njia moja ya kukumbatia jumuiya ya Afrika mashariki EAC baada ya DR Congo kujiunga na jumuiya hiyo mwaka uliopita.
Raia wa Kenya na DR Congo wako huru kutembea katika nchi hizo mbili bila vikwazo vyovyote.
Mataifa ambayo yameondoa hitaji la viza ili kuzuru Kenya ni pamoja na Indonesia Comoros, Senegal, Eritrea, Djibouti na Afrika Kusini.