Wakenya waliosajiliwa katika bima ya hospitali ya NHIF watalazimika kujisajili upya kwa bima mpya ya SHIF.
Akizungumza siku ya Jumamosi katika kaunti ya Bomet Rais William Ruto amefichua kuwa wizara ya afya ikiongozwa na waziri Susan Nakhumicha itazindua usajili wa kitaifa wa Wakenya kwa bima hiyo mpya.
Ruto amesema haya alipozindua ujenzi wa barabara ya Kyogong—Kapkesosio— Sigor—Longisa katika eneo la Chepalungu, kaunti ya Bomet.
Katika bima hiyo ya SHIF wakenya wenye pato la chini watachangia shilingi 300 kwa kila mwezi, huku wasioweza kulipia wakigharamiwa na serikali.