Wakenya kupata pasipoti kwa muda wa wiki tatu kuanzia Aprili

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya Uhamiaji imetangaza kuwa Wakenya wanaotuma maombi ya pasipoti kuanzia mwezi Aprili mwaka huu watakapata stakabadhi hiyo muhimu ndani ya majuma matatu.

Katibu katika idara hiyo Julius Bitok ametangaza kuwa tayari wamepokea vijitabu vya kuchapisha pasipoti huku wakitarajia vingine milioni moja katika muda wa majuma machache yajayo.

Bitok amekariri kujitolea kwa idara ya uhamiaji kuondoa mrundiko wa uchapishaji wa pasipoti katika muda wa siku chache zijazo.

Haya yanajiri siku chache baada ya Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki kukubali lawama ya kuchelewa kutolewa kwa stakabadhi hizo.

Share This Article