Wakenya kumenyana Berlin Marathon leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 50 ya mbio za Berlin Marathon yataandaliwa leo Septemba 29 nchini Ujerumani, huku kwa mara ya kwanza mshindi wa mashindano ya mwaka 2022 na 2023 Eliud Kipchoge akikosa kushiriki.

Mbio za wanaume zitawashirikisha wanariadha 14 ambao wamekimbia muda chini ya saa 2 na dakika sita.

Cybrian Kotut na Kandie Kibiwott ndio Wakenya walio na muda wa kasi wakijivunia saa 2 dakika 4 na sekunde 34 na saa 2 dakika 4 na sekunde 48 mtawalia.

Wakenya wengine watakaoshiriki ni Samuel Mailu,Justus Kangogo,Philimon Kipchumba,Asbel Rutto,Josphat Boit na Stephen Kiprop.

Wakenya watapata ukinzani mkali kutoka kwa Waethiopia Tadese Takele,Hailemaryam Kiros,Bazezew Asmare,Milkesa Mengesha na Haymanot Alew .

Veronica Maina na Pauline Esikon watakuwa Wakenya pekee watakaoshiriki huku wakishindana na Waethiopia Sisay Gola,Fikrte Wereta,Aberu Ayana,Bekelech Gudeta na Betelihem Afenigus.

Share This Article