Wakenya 63 wawasili nchini baada ya kuhamishwa na serikali kutoka Lebanon

radiotaifa
1 Min Read

Jumla ya Wakenya 63 waliwasili nchini wiki iliyopita baada ya kuhamishwa na serikali kutoka Lebanon kufuatia mashambulizi ya Israel.

Watu 40 waliwasili Alhamisi iliyopita katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta huku wengine 23 wakitua Ijumaa.

Oparesheni hiyo iliongozwa na idara mbali mbali za serikali kwa ushirikiano na Wizara ya wakenya wanaoishi ughaibuni.

Kufikia sasa takriban Wakenya 100 wamerejeshwa nchini kutoka Lebabon, baada ya kundi la kwanza la watu 39 kuwasili mapema mwezi huu.

Zaidi ya Wakenya 7,000 wamekwama nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya Israel yanoyoendelea nchini humo.

Share This Article