Wakazi wa Nakuru kupokea huduma za bure za matibabu

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya katika kaunti ya Nakuru watapata huduma za bure za matibabu baina ya Julai 4 na 7 ,baada ya kampuni ya Jubilee Health Insurance kuzindua mpango wa siku nne wa Afya Mashinani utakaondaliwa katika maeneo ya Naivasha na Nakuru.

Akizungumza alipozindua mpango huo afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Jubilee Health Insurance Njeri Jomo, amesema baadae wanapanga kueneza huduma hizo katika kaunti zote 47 nchini ambapo wakenya watapata huduma za uchunguzi wa kiafya,ushauri ,matibabu na chanjo ya ugonjwa wa Covid 19 bila malipo kwa ushikiano na Hospitali ya Aga Khan.

Njeri Jomo-Afisa Mkuu Mtendaji Jubilee Health Insurance

“Tunaamini upatikanaji wa rahisi wa huduma za kimatibabu kwa watu wote , bila kuzingatia misingi yao ya maisha .
Ni hii imani ambayo imetuchochea kuanzisha mpango wa Afya Mashinani utakaotoa huduma za matibabu kwa jamii zote nchini tukianzia maeneo ya Naivasha na Nakuru.”akasema Njeri Jomo

Mpango huo unalandana na ajenda ya serikali ya upatikanaji wa huduma nafuu za matibabu kwa Wakenya wote.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *