Wajumbe wa Sudan na UAE warushiana cheche katika kikao cha UNSC

Dismas Otuke
1 Min Read

Wajumbe wa Sudan na Ufalme wa Milki za Kiarabu, UAE walifarakana kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC siku ya Jumanne. Kiini cha mafarakano hayo kilikuwa shutuma za Sudan kuwa serikali ya UAE imekuwa ikiyapa silaha makundi hasimu yanayoipinga serikali katika mzozo ambao umedumu miezi 14 sasa.

Wakiwa wameketi pamoja, Balozi wa UAE katika Umoja wa Mataifa, UN Mohamed Abushahab alisema Balozi wa Sudan huko UN Al-Harith Idriss Al-Harith Mohamed alikuwa ametoa madai ya uwongo.

Mzozo ulizuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka jana na kwa mujibu wa takwimu za UN, takriban watu milioni 25 ambao ni nusu ya idadi ya watu wote nchini humo wanahitaji misaada ya kibinadamu huku wakikaribia kukumbwa na baa la njaa. Watu milioni nane wametoroka makwao.

Hata hivyo, UAE imekana madai ya kuegemea upande wowote katika mzozo unaoshuhudiwa nchini Sudan.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *