Wajane sio omba omba, asema Dorcas Rigathi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mke wa naibu wa Naibu Rais Mchungaji Dorcas Rigathi.

Mkewe naibu Rais Mchungaji Dorcas Rigathi, amekariri kuwa wajane sio watu wa kuomba omba bali ni wanawake waliojipata katika hali hiyo.

Akizungumza leo wakati wa kuzindua sera ya jinsia na maendeleo ya kaunti ya Nyeri na chama cha akiba na mikopo cha wajane katika afisi ya gavana, Dorcas aliwataka wajane washiriki miradi inayowaletea mapato, huku akiwataka kujinufaisha na miradi mbali mbali na fursa zinazotolewa na serikali ya kaunti ya Nyeri.

“Mume anapomuacha mke, haimaanishi mjane huyo sasa anapaswa kuwa omba omba, anauwezo wa kuwalea watoto wake,” alisema Mchungaji Dorcas.

“Maisha ya ujane si ya kujichagulia,” aliongeza Dorcas.

Mchungaji Dorcas aliwahimiza wajane kukumbatia miradi ya kuwaletea mapato, huku akiwatala kuchukua fursa ya fursa zinazotolewa na serikali ya kaunti ya Nyeri.

Alisema kuwa kuwawezesha kiuchumi wajane ndiyo njia ambayo vizingiti vyote vya kiuchumi, kijamii na kitamaduni vinaweza kuondolewa.

Kwa upande wake, gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga aliwahimiza wajane waungane ili kuboresha maisha yao kupitia vyama vya akiba na mikopo.

Aliahidi kuwasaidia wajane kwa kuwatengea mgao ambapo alikabidhi suala hilo kwa naibu wake David Kiranire ili kulishughulikia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *