Waisrael wapatao 22 wameuawa na kundi haramu la Hamas la Palestina ,kwenye shambulizi la mapema Jumamosi na kumlazimu Waziri mkuu wa Israel ,Benjamin Netanyahu kutangaza vita dhidi ya Palestina.
Kundi hilo lilivizia kambi ya wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza .
Kundi la Hamas limetekeleza shambulizi hilo kwa kutumia zaidi ya roketi 2,000 na kuwauwa watu 22 huku mamia wakijeruhiwa .
Mashambulizi hayo ya Roketi yalitekelezwa usiku kucha siku ya Jumamosi na kufikisha idadi ya zaidi ya roketi 2,500 ambazo zimetekeza mashambulizi dhidi ya Israel kufikia sasa.