Waislamu waadhimisha sikukuu ya Idd kote ulimwenguni

Mfungo wa Ramadhan ni mojawapo wa nguzo tano kuu za Uislamu, ambapo Waislamu hufunga kula na kunywa huku wakiomba.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jamiii ya Waislamu kote ulimwenguni wameadhimisha sikukuu ya Idd-Ul-Fitr kusherehekea kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Waislamu walimiminika katika misikiti kote nchini kwa ibada ya maombi kabla ya kujumuika na ndugu, jamii na marafiki kwa sherehe hizo.

Mfungo wa Ramadhan ulikamilika rasmi jana baada ya kuandama kwa mwezi kuashiria kuwa Waislamu walifunga kwa siku 29 mwaka huu.

Mfungo wa Ramadhan ni mojawapo wa nguzo tano kuu za Uislamu, ambapo Waislamu hufunga kula na kunywa huku wakiomba.

Sherehe hizi hujumuisha mlo wa pamoja, wakati familia na marafiki wanapokutana ili kusherehekea na kufurahia matunda ya ibada zao.

Wengi hujitoa kwa kutoa misaada kwa wenye uhitaji, kuonyesha roho ya ukarimu na mshikamano ndani ya jamii.

Hii ni fursa nzuri ya kuimarisha mahusiano na kufurahia urafiki, huku wakikumbuka umuhimu wa kusaidiana.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *