Waiguru ahifadhi uenyekiti wa Baraza la Magavana

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa Baraza la Magavana.

Waiguru amechaguliwa tena leo Jumatatu wakati wa uchaguzi wa Baraza Kuu na Kamati ya Kiufundi ulioandaliwa katika kaunti ya Nairobi.

Gavana Waiguru atahudumu kwa mara ya pili baada ya kuhudumu kutoka Disemba mwaka 2017 hadi Januari mwaka 2019 akiwa Naibu Mwenyekiti  wa kwanza wa kike wa baraza hilo  kabla   ya kuchagiliwa  kuwa mwenyekiti  mwaka uliopita.

Alimrithi aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Embu Martin Wambora.

Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi amechaguliwa kuwa Naibu Mwenyekiti huku Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja akipoteza kiti chake cha kuongoza Kamati ya Nguvu Kazi kwa  Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga.

Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti pia alibwagwa na Susan Kihika wa Nakuru ambaye sasa atahudumu kama mwenyekiti wa Kamati ya Biashara.

Share This Article