Wahandisi wapinga hatua ya kuondolewa kwa shuruti la Hisabati shuleni

Dismas Otuke
1 Min Read

Taasisi ya Wahandisi nchini imeondoa IEK, imepinga hatua ya Wizara ya Elimu kuondolea mbali somo la Hisabati, kuwa la lazima kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini.

IEK imesema kuwa Hisabati ni somo muhimu ambalo wanafunzi wote wanapaswa kulazimishwa kulifanya ilivyo kwa sasa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Rais wa IEK, Shammah Kiteme, wizara ya Elimu inapaswa kurejesha kigezo Hisabati kwa wanafunzi wote wanaopania kujiunga na vyuo vikuu nchini.

IEK imesema hisabati ni somo kuu kwa taaluma nyingi ikiwemo viwanda, kawi, miundo msingi na teknolojia ya habari na mawasiliano, na kamwe halipaswi kuwa la hiari kwa wanafunzi.

Badala yake, IEK imevitaka vyuo vyote vya kiufundi na vyuo vikuu kuweka kigezo cha somo la hisabati na sayansi kwa wanafunzi wote wanaotaka kusomea taaluma za sayansi na zile za kiufundi.

Wizara ya elimu wiki iliyopita itangaza kuwa wanafunzi wa gredi ya tisa hawatalazimishwa kusoma Hisabati, bali watachagua masomo kulingana na taaluma wanazopania kujiunga nazo.

Website |  + posts
Share This Article