Wahamiaji 23 wa kigeni wafikishwa mahakamani Marsabit

Wako Ali
1 Min Read

Wahamiaji haramu 23 raia wa Eritrea walifikishwa katika mahakama ya Marsabit hapo Jana kwa mashtaka ya kupatikana nchini bila stakabadhi za kuwaruhusu kuwa nchini.

Wahamiaji hao walikamatwa na maafisa wa polisi katika eneo la manyatta karatasi eneo bunge la saku kaunti ya Marsabit.

Miongoni mwa wahamiaji hao ni Wanaume 19 na wanawake 4.
Walifikishwa mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa kujibu mashtaka. Wote walikiri mashtaka dhidi Yao.

Hakimu Wekesa kupitia hukumu ya njia ya video aliwapata na hatia wahamiaji hao na kuwapiga faini ya elfu Arobaini au kifungo cha miezi mitano Kila Moja.

Wako Ali
+ posts
TAGGED:
Share This Article