Wahadhiri wamaliza mgomo wa siku 26

Dismas Otuke
1 Min Read

Wahadhiri na wafanyikazi wote wa vyuo vikuu vya umma  kote nchini watarejea kazini Jumatatu ijayo Novemba 25 ,hii ni baada ya chama cha UASU kutangaza kumaliza mgomo baada ya kuafikiana na serikali .

Chama cha UASU kimetangaza kuwa kimeafikia mwakafaka na serikali ambayo imetoa shilingi bilioni 9.7, katika makubaliano ya nyongeza ya mishahara mwaka 202 hadi 2025.

Katika maelewano hayo Wizara ya Hazina kuu imetenga shilingi bilioni 4.3 kwa mwafaka wa nyongeza ya mishahara mwaka 2024-2025, huku kiwango kilichosalia kikitekelezwa katika awamu mbili za shilingi bilioni 2.7 kila moja.

UASU na serikali pia wameafikiana kuondoa kesi zote zilizo mahakamani huku wafanyikazi wakitakiwa kurejea kazini Jumatatu ijayo.

Wahadhiri na wafanyikazi wote wa vyuo vikuu cya umma wamekuwa kwenye mgomo kwa muda wa siku 26 zilizopita.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *