Wagonjwa sita wa Ebola wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini huku Kenya ikikosa kurekodi kisa chochote ndani ya siku nane zilizopita.
Wizara ya afya imesema kufikia Ijumaa Novemba 6, ambayo ni siku ya 32 tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya Bundiburgyo,jumla ya wagonjwa sita wamepona na kuondoka hospitalini.
Mwanaume wa sita aliyekuwa akiugua ugonjwa wa Ebola ameondoka baada ya kutimiza masharti yote na kupatikana kutokuwa na virusi.
Aidha,watu 66 waliokuwa wametangamana na mgonjwa wa kwanza wameruhusiwa kuondoka baada ya kumaliza siku 21 za kujitenga.
Pia watu wengine 52 wangali wanazuiliwa wakiwa wamejitenga kufuatia kutangamana na mgonjwa wa kwanza .
Wagonjwa wote waliojitenga wanatarajiwa kufunguliwa ifikiapo Novemba 11.
Serikali imesema itaendelea kuchunguza abiria wote wanaoingia humu nchini kupitia kwa mipaka sita na pia uwanja wa Ndege wa JKIA .