Waganda milioni mbili kupokea chanjo ya HIV

Dismas Otuke
1 Min Read

Kama njia ya kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi ,serikali ya Marekani ikishirikiana na ile ya Uganda zinalenga kutoa chanjo ya HIV kwa raia milioni mbili.

Haya yanajiri huku taifa hilo likinakili visa 38,000 kwa mwaka huu licha kuwepo kwa uhamasisho na mbinu kadhaa za kuzuia maambukizi kama matumizi ya kinga na tembe za ARV.

Shirika la Global Fund kwa ushirikiano na shirika la Rais wa Marekani la kutoa misaada ya dharura kwa maambukizi ya ugonjwa wa HIV AIDS(PEPFAR), likisaidiwa na Wakfu wa Bill and Melinda Gates, limepanga kutoa chanjo hiyo kwa Waganda milioni 2 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Chanjo hiyo ijulikanayo kama Lenacapvir ilifanyiwa uchunguzi nchini Afrika Kusini na Uganda na kuthibitihswa kuzuia maambukizi mapya.

Kulingana na wataalam waliotengeza chanjo hiyo,vijana wa kike na kiume nchini Uganda watachanjwa mara mbili kwa mwaka kuanzia mwaka ujao, huku Marekani ikilenga kuafikia lengo lake la kumaliza maambukizi ya HIV nchini Uganda ifikiapo mwaka 2030.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *