Wafugaji Kitui wahimizwa kuwachanja mifugo wao

radiotaifa
1 Min Read

Eneo kubwa la Mwingi katika kaunti ya Kitui linajulikana kwa ufugaji wa mifugo kwa kiwango kikubwa, huku wakulima wengi wakianza kuachana polepole na kilimo cha mahindi na maharagwe kutokana na kushuhudia hasara ya mazao mara kwa mara.

Waziri wa Kilimo na Mifugo katika serikali ya kaunti hiyo Dkt. Stephen Mbaya Kimwele, amewahimiza wafugaji kuhakikisha wananufaika na chanjo zinazoendelea za mifugo dhidi ya ugonjwa wa midomo na kwato ili kuepuka hasara.

Pia amewataka wakulima kujipanga katika vikundi, huku wizara ikipanga kuwatafutia masoko ya mifugo yao.

Share This Article