Wafanyakazi wote nchini wanatarajia kupokea mishahara ya chini zaidi mwishoni mwa mwezi Agosti kufuatia agizo la serikali la kuanza kutekelezwa kwa ushuru wa nyumba.
Kufuatia agizo la matozo hayo kurejeshwa nyuma hadi Julai Mosi mwaka 2023, ina maana kuwa kila mfanyakazi atalipia matozo ya miezi miwili, katika mshahara wa mwisho wa mwezi wa Agosti ikiwa ni ujumuishaji wa ushuru wa mwezi Julai na Agosti.
Kila mfanyakazi anapaswa kukatwa asilimia 1 nukta 5 ya mshahara wa jumla kabla ya kukatwa ushuru kugharimia matozo ya nyumba kumaanisha kuwa wafanyakazi watakatwa asilimia 3 mwezi Agosti .
Wafanyakazi wanaopokea mshahara wa jumla wa shilingi 50,000 kabla ya ushuru watalipia matozo ya nyumba ya shilingi 1500 huku wale wanaopokea shilingi laki moja wakikatwa shilingi 3,000 mwezi wa Agosti.
Ushuru wa nyumba utagharimia ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na serikali.