Wafanyikazi 9 wa chama cha akiba na mkopo wanaswa kwa wizi wa shilingi milioni 160

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa ujasusi wamewatia mbaroni wafanyikazi tisa wa chama cha akiba na mikopo kwa tuhuma za kupotea shilingi milioni 160.

Wafanyikazi hao wa chama cha akiba na mikopo cha Njiwa Sacco, ambayo inamili huduma ya kitaifa ya ujasusi NIS walikamatwa kufuatia unguzi na msako ambao umekuwa ukiendesha na makundi ya wapelelezi.

Tisa hao wamafurushwa kutoka kwa chama hicho cha akiba na mikopo kwa makosa kadhaa yakiwemo kupanga njama ya kuiba,kushirikiana kutekeleza wizi,utepetevu,kughushi.kutoa stakabadhi bandia na nia kutekeleza uhalifu.

Wafanyikazi hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Septemba 25 kujibu mashtaka.

Washirika wengine watatu wametoweka na wanasakwa na polisi.

Share This Article