Wafanyakazi hewa wa umma 17,000 wamulikwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Jumla ya wafanyakazi hewa wa umma 17,000 wamemulikwa kwa kulipwa mishahara bila kufanya kazi.

Kulingana na ripoti ya Tume ya Utumishi wa Umma, PSC, wafanyakazi hao hewa ni wa kutoka mashirika mbalimbali ya serikali.

Baadhi ya mashirika yenye idadi kubwa ya wafanyakazi hewa  ni Ikulu, KBC na Kenya Railways.

Ikulu ina wafanyakazi hewa 156, wafanyakazi 1,689 wakiwa kwenye orodha ya kulipwa mishahara, ilhali ukaguzi wa watu uliofanywa ulikuwa na idadi ya wafanyakazi 1,533.

Shirika la Reli nchini Kenya, KRC, lina orodha ya wafanykazi 3,287 huku idadi ya waliokaguliwa ikiwa 2,026.

Shirika la Utangazaji nchini, KBC lilinakili wafanyakazi 231 ambao walikuwa kwenye orodha ya malipo bila kuwa na majukumu yoyote.

Wizara kwa jumla zilikuwa na wafanyakazi hewa 12,329 huku mashirika ya serikali yakinakili wafanyakazi hewa 2,486.

Vyuo vikuu vya umma vina wafanyakazi hewa  1,885, wengine 225 katika tume za  serikali na 75 katika mashirika mengine ya serikali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *