Kundi la kwanza la wafanyakazi wapatao 350 wa kampuni ya Kwale ya uchimbaji madini ya Base Titanium litafurushwa rasmi kazini mwezi ujao.
Hii ni kufuatia makataa yaliyotolewa na serikali ya usitishwaji uchimbaji madini hayo ifikiapo tarehe 31 mwezi huu.
Kampuni ya Base Titanium imetenga shilingi milioni 906.5 kuwafidia wafanyakazi hao ambao watafurushwa kwa awamu kadhaa.
Jumla ya wafanyakazi 1,600 wanatarajiwa kutimuliwa ifiakiapo mwezi Juni mwaka ujao, wakati kampuni hiyo itasitisha rasmi shughuli zote za uchimbaji madini ya Titanium.
Base Titanium imelazimishwa kufunga shughuli baada ya kumalizika kwa madini hayo humu nchini.
Kampuni hiyo imekuwa ikihudumu tangu mwaka 2013 ambapo imekuwa ikichangia asilimia 65 ya madini yote yanayouzwa nje ya nchi.