Waendesha bodaboda waandamana Mlolongo

Marion Bosire
1 Min Read

Wahudumu wa bodaboda wanaandamana katika eneo la Mlolongo, kwenye barabara kuu ya kuelekea Mombasa ambapo wamefunga barabara na kusababisha msongamano.

Maafisa wa trafiki wamelazimika kuelekeza magari kwenye barabara ya Express way kufuatia hali hiyo.

Kulingana na taarifa wanabodaboda hao wanalalamikia kile walichokitaja kuwa kuchomwa kwa pikipiki za wenzao kwenye maandamano ya jana dhidi ya serikali.

Pikipiki zipatazo tano zinadaiwa kuchomwa wakati wa maandamano jana katika eneo la Kitengela katika kaunti ya Kajiado.

Website |  + posts
Share This Article