Wadau watoa wito wa wanafunzi wasichana kupewa visodo

Martin Mwanje
1 Min Read

Ukosefu wa visodo kwa baadhi ya wasichana wa shule za upili na za msingi ndio umechangia sana kuongezeka kwa visa vya mimba za mapema na wasichana wengi kuacha masomo nchini.

Wakizingumza katika shule ya upili ya Kipkoror katika eneo bunge la Nandi Hills, kaunti ya Nandi, wadau katika sekta ya elimu na mashirika mbalimbali wameitaka serkali kusambaza visodo kwa shule zote nchini ili kuboresha hali ya masomo kwa wasichana.

Aidha wengi wao wanasema kuwa asilimia kubwa ya wasichana ambao huathirika zaidi ni wale wanaotoka kwa familia maskini na ipo haja kwa wabunge kuharakisha mswada unaonuia kuhakikisha usambazaji wa visodo kwa wanafunzi wote kote nchini.

Wanafunzi zaidi ya 600 walipewa visodo shuleni Kipkoror wakati wa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.

Share This Article