Wadau wa soka waitaka FKF kuitisha uchaguzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Wadau wa soka nchini wameitaka afisi ya sasa ya FKF kutoa arifa ya uchaguzi kabla ya muda wa sasa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Wakizungumza katika kaunti ya Nairobi siku ya Jumatatu, wakiongozwa na aliyekuwa afisa wa zamani wa shirikisho la KFF Noordine Taib, wadau hao pia wamemwomba Waziri wa Michezo Ababu Namwamba kuhakikisha maafisa wa sasa wa FKF wanafuata sheria na kuzingatia sheria za michezo mwaka 2013 na pia utekelezwaji wa ripoti ya msajili wa michezo ya mwaka uliopita.

Wadau hao wa soka wanatarajiwa  kufika mbele ya kamati ya michezo ya bunge la Seneti siku ya Jumanne  kuelezea mstakabali wa mchezo huo nchini.

“Soka yetu imerudi chini na tunataka Waziri wa Michezo Ababu Namwamba ahakikishe afisi ya sasa inafuata sheria  za michezo za mwaka 2013 na pia itoe arifa ya uchaguzi wa viongozi wapya kwani muda wao unakaribia kukamilika,” alisema Taib.

Kundi hilo linawashirikisha viongozi wa  vyama vya soka kutoka kaunti mbalimbali nchini wakiwemo James Bunei ambaye ni mwenyekiti wa Baringo, mwenzake wa Murang’a Daniel Maina na katibu wa chama cha soka katika kaunti ya Vihiga Peter Lisero miongoni mwa viongozi wengine.

 

 

Website |  + posts
Share This Article