Wachekeshaji wengi tu wa Kenya wamewasili jijini London nchini Uingereza kwa ajili ya tamasha ya vichekesho ya aina yake.
Wengi wamekuwa wakichapisha picha zao wakiwa safarini kuelekea Uingereza na hata wakiwa jijini London kwa ajili ya tamasha hiyo itakayoandaliwa Jumamosi, Septemba 2, 2023, katika ukumbi wa Royal Regency kuanzia saa 12 jioni saa za nchi hiyo.
Teacher Wanjiku, Jemutai, Profesa Hamo, YY na MCA Tricky ni kati ya wachekeshaji ambao watatumbuiza kwenye tamasha hiyo ambayo pia itajumuisha mwanamuziki Khaligraph Jones.
Tamasha hiyo imeandaliwa na shirikisho la wazaliwa wa Kenya wanaoishi Uingereza chini ya uongozi wake Prince Otach.
Tiketi za tamasha hiyo ya takribani saa 10 zilikuwa zinauzwa kwa Euro 30 sawa na shilingi elfu 4,697 za Kenya lakini bei hiyo ilikuwa iongezwe hadi Euro 60 sawa na shilingi 9,394 za Kenya kadri siku zilivyokuwa zikisonga.