Wachekeshaji maarufu humu nchini wataandaa tamasha ya kumkumbuka mwenzao aliyeaga dunia Fred Omondi ambaye ni kaka mdogo wa mchekeshaji Eric Omondi.
Kulingana na bango lililosambazwa mitandaoni, tamasha hiyo ambayo imepatiwa jina la “Fred Omondi Last Laugh” itaandaliwa Ijumaa Juni 21, 2024 katika mkahawa wa Carnivore jijini Nairobi.
Waliotajwa kwenye bango na ambao watatumbuiza siku hiyo ni pamoja na Churchill, Jalang’o, Profesa Hamo, Terrence Creative, Mamito, Nasra, Oga Obina, Captain Otoyo na wengine.
Kiingilio cha tamasha hiyo ni shilingi elfu moja.
Fred Omondi aliaga dunia katika ajali katika barabara ya Kangundo jijini Nairobi Jumamosi Juni 15, 2024 alfajiri akiwa amebebwa na pikipiki ya kusafirisha abiria almaarufu bodaboda.
Polisi walisema kwamba pikipiki hiyo iligongana ana kwa ana na basi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.