Wabunge wapitisha marekebisho kwenye Mswada wa Fedha 2024

Tom Mathinji
1 Min Read
Bunge la taifa.

Wabunge 195 leo Jumanne wamepiga kura na kupitisha marekebisho yaliyopendekezwa kwenye Mswada wa Fedha wa 2024, huku wabunge 106 wakiupinga mswada huo.

Mswada huo sasa unasubiri kusomwa mara ya tatu.

Mswada huo ulikuwa ukijadiliwa na kamati ya bunge lote baada kupitishwa uliposomwa mara ya pili juma lililopita.

Akitangaza matokea hayo, spika wa bunge la taifa Moses Wetang’ula, alisema kura tatu ziliharibika wakati wa mchakato huo.

“Matokeo ni kama yafuatavyo: Ndio 195, La 106, kura 3 ziliharibika,” alisema Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula.

Katika awamu ya tatu, hakuna marekebisho makubwa ambayo yatafanyiwa mswada huo.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *