Wabunge wajadili muswada wa uchimbaji dhahabu nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wameanza kujadili muswada wa 46 wa mwaka 2023 kuhusu kuanzishwa kwa taasisi na sheria za kudhibiti uchimbaji madini nchini.

Muswada huo pia unalenga kubuni sheria za kusajili kampuni za kuchimba, kusafisha, kuyeyusha na kusafirisha bidhaa za dhahabu.

Muswada huo wa mbunge wa Ikolomani Bernard Shinali, unalenga kuwezesha kuwa na akiba ya kutosha ya dhahabu nchini.

Tayari muswada huo umesomwa kwa mara ya pili na pia utabuni sheria za kuzuia uharibifu wa mazingira unaofanywa na kampuni za uchimbaji dhahabu na kuzuia uchimbaji haramu wa dhahabu.

Mjadala wa musuada huo utaendelea wiki ijayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *