Wabunge kutoka kaunti ya Mombasa wamelaani hatua ya polisi kufyatua vitoa machozi katika shule ya Coast Girls Jumatano wiki hii.
Wabunge hao wakiongozwa Mishi Mboko wa Likoni na mwakilishi wa wanawake Mombasa Zamzam Chimba, wametaka uchunguzi dhidi ya polisi waliohusika katika kisa hicho.
Polisi walilazimika kuwarushia waandamanaji vitoza machozi ilu kuwatawanya baada ya kufurika nje ya kituo cha polisi cha Central.
Waandamanaji hao walikuwa wakipinga mswaada wa fedha wa mwaka 2024, uliopitishwa na bunge juma hili.