Wabunge kupewa afisi mpya Bunge Tower

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wapatao 42 wanatarajiwa kukabidhiwa afisi mpya katika jengo jipya la Bunge Tower, kuanzia leo, baada ya ujenzi kukamilika.

Sehemu ya jengo hilo imekuwa ikitumika kwa vikao vya kamati za bunge tangu kuanza kwa bunge la 13.

Wabunge hao 42 watakaokabidhiwa afisi ni wale watakaohamishwa kutoka jumba la KICC.

Kulingana na Spika wa Bunge kitaifa Moses Wetang’ula, wabunge watahamia afisi mpya kwa awamu wakianza na 42 kutoka KICC.

Yamkini jengo hilo litafunguliwa rasmi baadaye mwezi huu na Rais William Ruto.

Share This Article