Waaniaji saba wameidhinishwa kuwania Urais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC),uchaguzi ulioratibiwa kuandaliwa wakati wa kikao cha 143 kati ya Machi 18 na 21 mwaka ujao nchini Ugiriki.
Saba hao ni pamoja Rais wa kamati ya Olimpiki nchini Uhispania Juan Antonio Samaranch aliye na umri wa miaka 65 na ambaye amekuwa mwanachama wa IOC tangu mwaka 2001.
Prince Feisal Al Hussein ambaye ni mwanawe Mfalme wa Jordanna ambaye amekuwa mwanachama wa IOC tangu mwaka 2010,Johan Eliasch ambaye ni Rais wa shirikisho la mchezo wa kuteleza kutoka Uingereza ,Rais wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni Lord Sebastian Coe wa Uingereza pia wanawania kiti hicho.
Wengine walio kinyang’anyoroni ni Rais wa shirikisho la uendeshaji baiskeli ulimwenguni David Larppatient kutoka Ufaransa,Rais wa shirikisho la mchezo sarakasi Moninare Watanabi kutoka Japan na mwaniaji pekee wa kike Kirsty Coventry ambaye ni makamu rais wa kamati ya Olimpiki ya Zimbabwe.
Saba hao walituma maombi yao kufikia jana Septemba 15 ambayo ilikuwa siku ya mwisho huku wakilenga kumrithi Mjerumani Thomas Bach, kutoka Ujerumani ambaye alitangaza kutotetea kiti hicho.
Bach ni Rais wa tisa wa IOC na bingwa wa kwanza wa Olimpiki kuhudumu katika kiti hicho.