Waandamanaji wavamia afisi ya mbunge wa Nyali

Francis Ngala
2 Min Read

Kundi la waandamanaji wanaopinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024 leo Jumatatu walivamia afisi ya mbunge wa Nyali Mohamed Ali kuwasilisha na kuelezea kutoridhishwa kwao kutokana na madai ya mbunge huyo kushindwa kutangaza msimamo wake kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka 2024.

Ali hakuwepo katika Bunge la Taifa wakati wenzake walipokuwa wakipiga kura ya Ndio au La kwa ajili ya mswada huo kusomwa kwa mara ya pili.

Kundi hilo la vijana liliandamana hadi afisini mwake eneo bunge la Nyali, kaunti ya Mombasa kwa nia moja tu ya kufahamu iwapo mbunge wao anaunga mkono mswada huo au la.

Mwandamanaji mmoja kwa jina Lydia Adhiambo, akiongea na wanahabari alisema wasiwasi wao ni kuwa mbunge huyo angali kutangaza msimamo wake kuhusu suala hilo.

“Tunamletea salamu Mohamed Ali, kwa nini amenyamaza wakati Mswada wa Fedha 2024 unaathiri kila eneo la nchi? Hatukumuona bunge akipiga kura, na kunyamazwa kwake inaashiria anakubaliana nao,” alidai Lydia.

Mwandamanaji huyo pamoja na kundi la wenzake walisisitiza kwamba mbunge wao hana chaguo lingine bali tu kuridhia msimamo wa kupinga mswada huo.

Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, haikuwa wazi iwapo mbunge huyo alikuwa afisini au hakuwepo kwani lango kuu la kuingia afisini humo lilifungwa na waandamanaji hawakuruhusiwa kuingia.

Website |  + posts

I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.