Waandamanaji walalamikia uhusika wa Iyabo katika uchunguzi wa kifo cha Mohbad

Wanadaiwa kufadhiliwa na watu fulani ambao huenda wakafahamu yaliyomfika Mohbad na kusababisha kifo chake.

Marion Bosire
2 Min Read
Iyabo Ojo

Watu wapatao sita leo walionekana wakifanya maandamano kwenye barabara za jimbo la Lagos nchini Nigeria, wakilalamikia uhusika wa mwigizaji Iyabo Ojo kwenye uchunguzi wa kifo cha mwanamuziki Mohbad.

Wanaume hao sita walisikika wakifoka maneno ya kumlaani Iyabo na wengine wanaohusika na uchunguzi huo. Haya yanajiri saa chache tu baada ya moto kuteketeza sehemu ya afisi za Iyabo Ojo.

Mashabiki wa mwigizaji huyo mitandaoni wamegawanyika kuhusu tukio hilo ambapo wengine wanalalamikia hatua ya waandamanaji hao huku wengine wakimlaumu kwa kujiingiza kwenye uchunguzi isiomhusu.

Wakili wa May Edochie aitwaye Emeka Ugwuonye, alikuwa amefichua awali kwamba kuna watu wanampangia mabaya Iyabo Ojo kwa kuhusika na uchunguzi huo.

Ugwuonye aliendelea kwa kumshauri Iyabo kuhusu hatua anazostahili kuchukua.

Iyabo Ojo, kupitia Instagram amezungumza kufuatia tukio la jana na la leo akisema polisi walimhusisha na uchunguzi wa kifo cha Mohbad kufuatia video aliyochapisha mitandaoni wakati wa kifo cha mwanamuziki huyo ambapo alitaja wanaofaa kuchunguzwa kuhusiana na kifo chake.

Ojo anasema aliitikia wito wa polisi, amekuwa akisaidia katika uchunguzi lakini hana udhibiti wa hatua ambayo huenda maafisa wa usalama wakachukua.

Anasema alipokuwa nchini Tanzania kuhudhuria harusi ya binti yake Priscilia aliyeolewa na mwanamuziki Juma Jux, alipokea barua ya vitisho iliyodai kwamba atakuwa na wakati mgumu sana katika muda wa miezi mitatu.

Website |  + posts
Share This Article