Vivian Cheruiyot kurejea uwanjani Jumapili kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili

Dismas Otuke
1 Min Read

Vivian Cheruiyot atarejea uwanjani kwa mara ya kwanza Jumapili kutimka mbio za barabarani za kilomita 15 za NN Zevenheuvelenloop mjini Nijmegen nchini Uholanzi.

Bingwa huyo wa dunia mara mbili amekuwa kwenye likizo ya zaidi ya miaka miwili tangu ajifungue .

Cheruiyot aliye na umri wa miaka 40 kwa sasa anajishughulisha na mbio za barabarabi na marathoni.

Katika mashindano ya Jumapili Cheruiyot maaaru kama Pocket Rocket atapambana na mshikilizi wa record ya dunia ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji beatrice Chepkoech.

Website |  + posts
Share This Article