Vitambulisho vya kitaifa zaidi ya 13,000 havijachukuliwa Murang’a

Tom Mathinji
1 Min Read

Vitambulisho vya kitaifa zaidi ya 13, 000 havijachukuliwa katika afisi za usajili wa watu, kaunti ya Murang’a.

Msajili wa watu wa kaunti hiyo Juliet Mutitu, amesema baadhi ya vitambulisho hivyo havijachukuliwa tangu mwaka 2010.

Kulingana na Mutitu, kaunti ndogo ya Murang’a kusini, inaongoza ikiwa na vitambulisho 2,099 ambavyo havijachukuliwa.

“Murang’a Kusini inaongoza kwa idadi kubwa ya vitambulisho ambavyo havijachukuliwa,” alisema Mutitu.

ili kutatua swala hilo, Mutitu alisisitiza haja ya kushirikiana na maafisa wa serikali ya taifa ikiwa ni pamoja na machifu na manaibu wao kuwahimiza wanaotuma maombi, kuzichukua punde zinapotoka.

Aidha alisema baadhi ya sababu ya kutochukuliwa kwa vitambulivyo hivyo, ni watu kuhama kutoka eneo moja hadi lingine, vifo au kutojali.

“Baadhi ya watu huhama kabla ya kuchukua vitambulisho vyao. Wengine huaga dunia, huku wengine wakipuuza tu,” aliongeza Mutitu.

TAGGED:
Share This Article