Timu ya Taifa ya soka ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 imekaribia kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia,baada ya kuibwaga Ethiopia magoli matatu Kwa nunge Jumapili jioni ugani Ulinzi Complex .
Elizabeth Ochaka alipachika bao la kwanza kwa watoto wa nyumbani kunako kipindi kwanza kupitia kwa mkwaju wa Kona.
Kwenye kipindi cha pili, Velma Awor na faith Lorna walizidisha machungu Kwa Wahabeshi walipovurumiza makombora mazito yaliyomwacha hoi mlinda lango na kufanya mambo kuwa tatu bila.
Ushindi huo umeivusha Kenya hadi raundi ya nne na ya mwisho ambapo watachuana na Burundi tarehe 7 na 14 Juni katika mkondo wa kwanza na wa pili.
Iwapo Kenya itashinda awamu hiyo, itafuzu Kwa kombe la dunia Novemba mwaka huu katika Jamhuri ya Dominika.