Viongozi wa mashtaka wakataa kumshtaki Rais Ramaphosa

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Viongozi wa mashtaka nchini Afrika kusini wamesema kuwa hawatamfungulia Rais Cyril Ramaphosa mashtaka ya uhalifu kuhusiana na sakata ya wizi wa shamba ambayo nusura yasambararishe utawala wake miaka miwili iliyopita.

Afisa mmoja mkuu wa zamani wa ujasusi aliwasilisha malalamishi ya kiuhalifu dhidi ya Ramaphosa, akimshtumu kwa kutenda makosa katika kujaribu kuficha wizi wa dola milioni nne za kimarekani pesa taslimu kwenye shamba lake la wanyama pori katika jimbo la Limpopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Rais huyo alikanusha kutenda kosa lolote akisema kuwa pesa zilizoibwa kutoka kwenye kiti chake mwaka 2020 zilitokana na uuzaji halali wa nyati kwenye shamba lake la Phala Phala.

Ramaphosa alinusurika kwenye sakata hiyo na kuchaguliwa tena kuwa rais mwezi Juni na kulazimika kubuni muungano huku uchunguzi wa kiuhalifu ukiendelea.

Mnamo mwaka 2022, chama chake cha African National Congress (ANC) kilitumia wingi wa wabunge wake kuzuia hoja ya kumwondoa afisini dhidi yake kuhusiana na sakata hiyo.

Website |  + posts
Share This Article