Baadhi ya viongozi wa kisiasa hapa nchini, wamekosoa mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya vyuo wakisema kuwa unawanyima wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo kutokana na vikwazo vya kifedha.
Wakizungumza na wanahabari Alhamisi, viongozi hao waliojumuisha Kabando wa Kabdando, Mukhisa Kituyi, Prof Kibutha Kibwana na Martha Karua, sasa wanaitaka serikali kurejelea ufadhili wa awali ikisubiri kuamuliwa kwa kesi ya kupinga utekelezaji wa mfumo huo mpya.
“Serikali ya Rais Ruto inacheza na moto kwa kusambaratisha mfumo katika viwango vyote,” alisema kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.
Kulingana na Karua, usimamizi wa serikali wa mpito wa mfumo huo umewaathiri zaidi wanafunzi.
Wanasema kuwa kuna ubaguzi na ukosefu wa usawa katika kuwagawanya wanafunai hao katika kategoria mbalimbali hali inayotishia kuwafungia nje wanafunzi kutoka familia maskini kupata elimu ya juu.
Viongozi hao wametoa wito wa juhudi za pamoja za kutafuta suluhu kwa mzozo wa ufadhili wa elimu ya juu.
kadhalika wanaitaka serikali kutimiza wajibu wake na kutekeleza mkataba wa makubalianao ya pamoja waliotia saini na wahadhiri ili masomo yarejelewe katika vyuo vikuu.