Viongozi wa Dini ya Kiislamu wamewataka wakenya kuweka amani na kujitenga kutoka kwa mirengo ambayo huenda ikawagawanya kwa misingi ya kisiasa.
Wito huu wa viongozi una ujio wakati ambapo Joto la siasa humu nchini linazidi kupanda, viongozi wakitupiana maneno siku baada ya nyingine.
Wakiongea kwenye Hafla ya Kusherehekea kuzaliwa kwa mtume Muhammad, viongozi hao wa kidini Wakiongozwa na Sheikh Mohamed Bilal Laving wamewataka wakenya kukumbatia umoja na undugu katika kukuza Taifa lenye uwiano na utangamano wa kitaifa.
“Jamii nzima na ndugu zetu wakenya tuungane na tukuze taifa letu kwa pamoja” Sheikh Mohamed akasema.
Cheche za maneno kati ya Naibu Rais na wandani wa Rais siku za hivi majuzi zimewaacha wengi kutilia shaka imani ya viongozi hao ambao walitumia ukristu kupata nyadhifa zao za sasa.