Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Kaloleni

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Mombasa.

Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI, wamewakamata washukiwa watatu wa ulanguzi wa mihadarati eneo la Kaloleni kaunti ya Mombasa.

Kupitia mtandao wa X, idara ya DCI ilisema kuwa watatu hao walitiwa nguvuni baada ya wananchi kuwapasha habari maafisa hao wa polisi.

Juma Nyiro Wanje, Wanje Nyiro Wanje na Francis Arome Chiringa, walifumaniwa na maafisa hao wa polisi wakiwa na magunia sita ya bangi.

Baada ya kupokea habari za kijasusi,  maafisa hao walianzisha operesheni katika kijiji cha Birya, kaunti ndogo ya Kaloleni ambapo watatu hao walinaswa katika nyumba ya Juma Nyiro Wanje.

Bangi hiyo inashukiwa ilikuwa ikisafirishwa kuelekea Bamburi. Watatu hao wanazuiliwa na polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *